Eric Omondi Asherehekea Baada ya Ezekiel Mutua Kufutwa Kazi: "Nilimwambia"

July 2024 ยท 2 minute read

Mcheshi Eric Omondi na Ezekiel Mutua wamekuwa mahasimu kwa muda mrefu. Katika siku za hivi karibuni mcheshi huyo aliahidi kuanzisha kampeni ya kumtimua Mutua afisini kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Eric alimuonya Mutua kwamba anapaswa kuwaomba msamaha hadharani wasanii au aanzishe kampeni ya kumfurusha afisini.

Kwenye ukurasa wake wake wa Instagram msanii huyo alisema kwamba chuma cha Mutua katika afisi ya KFCB kiko motoni na huenda asifike Septemba.

Baada ya kugundua kuwa Mutua ametumwa kwa likizo ya lazima, Eric alichapisha ujumbe kwenye Instagram kusherehekea habari hiyo.

Alithibitisha chapisho lake la awali, ambalo lilikuwa limemuonya Mutua kwamba hatahudumu ofisini kwa muda mrefu labda hadi Septemba ikiwa hatawaomba radhi wasanii kwa matamshi yake makali.

Pia soma

Ezekiel Mutua Akanusha Madai Kwamba Amefutwa Kazi

Hata hivyo, alielezea shauku kuhusiana na habari hizo na kumshauri kwamba endapo sio ya kweli basiitakuwa vyema endapo ataomba radhi na kubadilisha mienendo yake.

"Nilisema hautafika Septemba na ulidhani ni utani. Huwezi kuuma mkono unaokulisha. Nilikuambia njia pekee ya kuponea shoka ni kuwaomba msamaha wasanii. Sina hakika iwapo taarifa zinazosambaa ni za kweli, lakini iwapo sio za kweli, basi bado utatemwa nje kabla ya Septemba kama nilivyoahidi usipoomba msahama na kurekebisha mienendo yako," aliandika Eric.

Awali, TUKO.co.ke iliripoti kuwa Eric alidokeza kwamba Mutua ameshindwa kufanya majukumu yake katika afisi ya KFCB.

Mcheshi huyo alinukuliwa akizungumza wakati wa mahojiano na kituo cha radio cha Empire FM huko Tanzania ambapo alisema Mutua amekuwa akimuandamana.

Aliongeza kwamba ataanzisha kampeni ya kuhakikisha Mutua amefutwa kazi kabla ya mwezi Septemba.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Pia soma

Gavana Mutua Adai Ruto Ameangusha Nchi Akiwa Kama Naibu Rais

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ352fJNmnKuhk2K8rrvNnaBmmaOdsrOxx56inpldl66isMBmsJplla%2ByrLXEpWSmraSqrm631J%2Bsra%2BRYriixshmpaKkmaLEornBophnoKSiuQ%3D%3D