- Naibu Rais William Ruto amejitenga na madai ya kutowajibikia ahadi walizowaahidi Wakenya akiwa na Rais wakati wa kampeni
- Ruto alidai kwamba amekuwa akipitia changamoto nyingi tangu uchaguzi mkuu wa 2017
- Kulingana na Ruto, alifanikiwa kufanya kazi kikamilifu muhula wa kwanza akiwa madarani
Naibu Rais William Ruto amekiri kwamba mambo yalianza kuzidi unga pindi tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.
Habari Nyingine: Jonathan Mukundi: Rafiki wa Familia Afichua Sabbau ya Hasira Iliyosababisha Mauaji

Habari Nyingine: Mbunge Rigathi Gachagua Adai Alitumia Mamilioni ya Pesa Kumpigia Kampeni Uhuru
Ruto aliiambia runinga ya Inooro Jumatano, Agosti 4, kwamba baada uchaguzi wa 2017 amekuwa akikumbana na changamoto nyingi zingine zilizopelekea yeye kupigwa teke na wandani wa Rais.
MAKINIKA: Jinyakulie habari ZINAZOKUFAA ➡️ tafuta “IMEPENDEKEZWA KWA AJILI YAKO” na ufurahie!

Pia soma
Ruto Abebwa Kama Hasla Uingereza, Raila Aanza Kupoteza Umaarufu na Matukio Mengine Wiki Hii
Aidha, Ruto amejitenga na madai ya kutowajibikia ahadi walizowaahidi wakenya akiwa na Rais wakati wa kampeni.
Ruto pia ameshikilia shaka maridhiano ya rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga machi 2018 almaarufu 'handshake'.
"Labda uwe mgeni Kenya hii, niliambiwa nikae kando, na kulikuweko na waliokuja kumsaidia rais wakiwemo watu wa NASA waliokuja kusambaratisha mipango yetu ya chama (Jubilee party)" alisema Ruto.
"Naliweza kuwaajibikia Wakenya kwa miaka mitano ya kwanza kikamilifu kama naibu wa rais." Aliongeza Ruto.
Haya yanajiri siku chache baada ya seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kudai kwamba Ruto ni naibu kikatiba lakini anayeendesha shughuli zake ni kinara wa ODM Raila Odinga.
Murkomen alikuwa akijibu kuhusu ni nani anayefaa kulaumiwa kwa kutotimiza ahadi za Jubilee.
Habari Nyingine: Fanta Jallow: Mrembo Kutoka Gambia Asafiri Hadi Kenya Kumtafuta Mamake
"Unaweza mlaumu Ruto kwa mambo ambayo yametendeka miaka minne iliyopita? Yeye sio mmoja wa viongozi serikalini, yeye yupo kikatiba tu lakini naibu wa rais Kenyatta ni Raila Odinga." Alisema

Pia soma
Hussein Mohamed Afurahia Kazi Yake Marekani Pamoja na Rais
Miezi michache iliyopita Ruto alikiri kwamba amehujumiwa kama naibu wa rais na hangependa mtu mwingine kuhujumika kwa njia hiyo.
"Nikipewa nafasi singependa kuona mtu mwingine akipitia yale napitia kama naibu wa rais." Ruto alisema katika runinga ya Inoor,"
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ35zgpRmrqKknJ6urnnRrquoZZGgtrO1jJqjop6Ro8aiecqasaJlm564ornIpaCfrV2gxKJ5zKKYpJldora1rc2oZLKZXaDEorrZmmSmmZSWv6K3wKegZ6Ckork%3D