Aliyekuwa mbunge wa Starehe Margaret Wanjiru amezungumza kwa mara ya kwanza tangu alipolazwa hospitalini baada ya kupatikana na COVID-19.
Aliwahutubia waandishi wa habari katika hospitali ya Aga Khan Jumamosi, Mei 30, askofu huyo alifichua kwamba alienda hospitalini pasi na kujua alikuwa ameambukizwa virusi hivyo hatari.
Habari Nyingine: COVID-19: Visa 143 vyathibitishwa, mtoto wa mwezi mmoja miongoni mwao

"Nilianza kuumwa na tumbo Jumamosi. Wakati nilienda hospitali sikueunda huko sababu ya COVID-19, sikuwa napiga chafya wala kukohoa, lakini sasa nimeondoka hospitalini nikiwa sina COVID-19 tena," alisema.
Habari Nyingine: Hali ngumu ya uchumi yafanya pasta ageukie utapeli
Wanjiru alilazwa hospitalini Alhamisi, Mei 21 na kuripotiwa kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Aga Khan University.

Wakati huo, uvumi ulisambaa kwamba mchungaji huyo ambaye pia ni mwanasiasa alikuwa na wageni bomani mwake, madai ambayo alipinga vikali.
Habari Nyingine: Siasa ni kujipanga: Mudavadi akutana na PK, Karua na Sally Kosgei
Alisema alikuwa na wajukuu wake wawili ambao pia walidhibitishwa kuambukizwa virusi hivyo hatari.
Alitoa wito kwa wananchi kutilia maanani maagizo ya serikali ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona akisema ni jukumu letu sote kuhakikisha ugonjwa huo unakabiliwa.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaoZ6fphmmKyjn5vCbrnAq56aqpWperitzaOgq61dlryvsM6kmGagn6i9qsDApaCnoV6dwa64