- Gavana wa Mombasa Hassan Joho anazidi kukejeliwa na baadhi ya viongozi kuhusiana na matokeo yake ya mtihani wa kitaifa wa KCSE
- Wafuasi wa mpinzani wake wa Hassan Omar walitaka walilinganishe vyeti vya masomo wa viongozi hawa wawili
- Huku omari akiwa alipata alama ya A- katika mtihani huo, Joho alipata alama ya D- mwaka wa 1993
Gavana wa Mombasa Hassan Joho anazidi kukejeliwa hadharani kufuatia matokeo yake ya mtihani wa kitaifa KCSE ambapo alipata alama ya D-.
Habari Nyingine: Mtaliano anaswa akimuangalia MKEWE Rais Uhuru kwa macho ya "kuzinguwa" (picha)
Habari Nyingine: Maajabu! Mwanamke ajifungua mapacha, mmoja wao ni NYOKA (picha)
Wafuasi wa Hassan Omar walimkejeli Joho kwa kuweka mitandaoni picha ya vyeti vya KCSE vya Omar na Joho sambamba ambapo Hassan alipata alama ya A-
Wafuasi hao waliweka picha hiyo kwa lengo la kumuaibisha Joho lakini la kushangaza Wakenya walikuwa na maoni tofauti.
Itakumbukwa kuwa Joho pia alipitia wakati mgumu alipokuwa katika harakati za kuwasilisha stakabadhi zake kwa tume huru na mipaka IEBC.
Habari Nyingine: Samuel Abisai, mshindi wa KSh 221 milioni za Sportpesa, anunua GARI la kifahari (picha)
Msimamizi wa kura kaunti ya Mombasa,Nancy Wanjiku alimushinikiza gavana huyo kuwasilisha cheti chake cha KCSE,jambo ambalo Joho alitaja kama kinyume na sheria.
“Tafadhali usibuni sheria yako, hakuna mahali imeandikwa kwamba cheti cha KCSE lazima kiwasilishwe kwa tume ya uchaguzi bali na cheti cha shahada,”Joho alinukuliwa na Nation
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaX93fZhmpKmZnpy8bsPAZqKupaWgsquxy6JkoZmjqK6vecmon6hlmJaxqa3RmqWiZZuqtba%2FyJqlmmWelnqurdOoop6nXa6urLGMsphmpaSetW%2B006aj